Kipindi cha Kwanza
Katika 3-2-3-2 ya Al Ahly mpango wao ni kushambulia zaidi kupitia watu wa pembeni (kulia ni El Shahat na Ally Maaloul wakati kushoto ni Mohamed Hany na Percy Tau) pia wakipata nafasi katikati wanamtumia Mohamed Afsha anayecheza mbele ya Dieng na Attia lakini ikawa ngumu. Kwanini?
Simba walitumia 5-3-2 (Hapa Ngoma na Saido mmoja alirudi chini) ili kuzuia kwenye “Low Block” ambayo iliwalipa kwa asilimia kubwa hasa kwenye mambo matatu…
1. Kushinda mipira ya juu na inayodondoka mbele ya eneo la ulinzi! kwenye eneo lao la kumi na nane (Mahmoud Kahraba akakosa uhuru wa kucheza kwenye nafasi za wazi hasa mbele ye Che Malone na Inonga).
2. El Shahat na Percy Tau kutopata nafasi ya kucheza ndani ya “Half Spaces” pia kufanya “Cut in” na wabaki kupiga krosi ambazo walinzi wa kati wa Simba walishinda nyingi.
3. Kuzuia Afsha kupokea mpira akiwa huru nyuma ya Ngoma na Kanoute pia kuwanyima nafasi ya kupiga sana mbele ya 18 yao.
Simba mpango wa kuzuia ukafanikiwa sana, wakawauliza safu ya ushambuliaji ya Al Ahly maswali mengi sana. Mbele John Bocco mikimbio yake ikawa dhidi ya AbdelMonem na Ramy Rabia.
Kipindi cha Pili
Jean Baleke anaingia na John Bocco anatoka shape ya Simba inakuwa 4-1-4-1 mpango wao ukiwa ni kucheza juu zaidi (Watu wanne nyumba, halafu Ngoma nyuma ya Chama, Saido, Kanoute na Kibu mbele Jean Baleke.
Simba mpango wao ukafanikiwa wakapata goli lakini pia ndio wapo hatarini. Kwanini?
1. El Shahat na Percy Tau kukimbia “Half Spaces” hapa Hany na Maaloul wakatumia nafasi zilizoachwa nyuma yao (Goli la kwanza).
2. Afsha akawa huru kupokea mpira karibu na 18 ya Simba, mikimbio yake ikawavuruga Che Malone na Inonga Bacca.
Simba mpango wao wa kukabia juu hapa uliwapa faida, kilichokuja kuamua ni Al Ahly kutengeneza nafasi bora na kuweka ugumu mechi.
Jicho la Tatu
• Maaloul usiache akapiga V passes zake zile ni hatari! El Shahat bonge la mchezaji! Mohamed Hany, yupo vizuri sana mguuni, mlinzi wa pembeni wa boli.
• Fabrice Ngoma utulivu na usahihi wake ni hatari! Che Malone safi kabisa! Inonga mtu kweli! Sadio Kanoute kaubonda sana
• Mahmoud Kahraba mikimbio yake na anavyojiweka katika nafasi ni hatari! Ntibazonkiza safi.