Kampuni ya usafirishaji wa mizigo Silent Ocean “Simba wa bahari” wamezindua michuano ya mpira wa miguu itakayofanyika wakati wa mwezi wa mfungo wa Ramadhani maarufu kama Ramadhan Cup.
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi wiki ijayo ambapo kwa mwaka huu itakua tofauti na miaka ya nyuma itaboreshwa zaidi na kuongeza msisimko wake.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha masoko Silent Ocean Mohamed Kamilagwa amesema malengo yao kwa mwaka huu ni kuibua vipaji, kujenga afya, kutoa burudani na kurudisha kwa jamii
Mohamed Kamilangwa “Lengo letu kuu ni kurudisha kwa jamii na kujumuika kwa pamoja lakini pia tungependa kuvumbua vipaji ambavyo bado havijaonekana na wapo huku mtaani.
Kamilangwa amesema pia wanashirikiana na mamlaka za soka mkoa na nchi pia katika uendeshaji wa mashindano hayo ambayo yataanza wiki ijayo na kutumia siku 29 katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park.
“Tunashirikiana na DRFA pamoja na TFF katika uendeshaji wa mashindano haya na pia yatafanyika katika viwanja vya JMK Park pale kidongo chekundu yakitumia siku 29 mpaka kukamilika kwake.
Kutakua na makundi matano yenye timu nne maana yake timu shiriki ni 20. Tunawakaribisha makampuni na taasisi mbambali waje wachukue fomu ofisini kwetu pale Lumumba,” alisema Kamilangwa.
Pia mashabiki hawakuachwa nyuma kwani kutakua na vifurushi kutoka Simba wa Bahari kwa wote ambao watakua wanahudhuria michuano hiyo itakayokua inafanyika nyakazi za usiku wakati wa mfungo.