- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
March 24 ya mwaka 2019 ni siku ambayo Taifa lilikua “busy” kwa asilimia kubwa ya Watanzania wapenda soka na wasio wapenda soka. Ilikua ni siku siku ya mwisho ya wiki iliyoanzishwa Jumatatu ya tarehe 19 ambapo Tanzania yote ilikua na mawazo yanayofanana.
Tangu March 19 nchi ilianza kua tofauti huku ikiwa na azimio moja tu lililokua likiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda huku akiwa na baadhi ya watu maarufu nchini wasanii wa sanaa za uimbaji na maigizo.
Walikuepo kina Mwana fa, JB,Wema Sepetu, Salama, Haji Manara na wengine wengi ambao walikua chini ya kamati ya Mkuu wa Mkoa wakiwa na lengo moja tuu la kuipeleka Tanzania katika michuano ya Afcon 2019 nchini Misri. Baada ya Tanzania kuikosa michuano hii kwa miaka 39 pengine huu ndo ulikua wakati sahihi wa kurudi tena katika michuano mikubwa Africa.
March 24 ikafika na watu elfu sitini walijitokeza kwenda kutimiza ndoto ya Watanzania zaidi ya milioni 50 pale Kwa Mkapa. Ni Tanzania na Uganda katika mchezo wa mwisho wa Kundi L. Huku Tanzania ikihitaji ushindi pekee katika mchezo huo ili kuweza kutimiza ndoto za kwenda Misri.
Wachezaji wa Taifa Stars waliingia uwanjani huku wakijua wana deni mbele ya Watanzania 60,000 waliopo uwanjani na Watanzania zaidi ya milioni 50 waliopo nyumbani. Na hata sura zao zilionyesha hilo wakati wanaimba mwimbo wa Taifa.
Dakika 90 zinamalizika Tanzania 3 Uganda 0, shukrani kwa Msuva, Nyoni na Morris waliopeleka kilio Kampala, halafu Tanzania inafuzu Afcon pale Misri baada ya miaka 39 tulipopelekwa na kina Peter Tino.
Ni moja ya siku ya furaha katika katika maisha yangu ya mpira hasa kwa Taifa langu. Siku ambayo naishuhudia timu ya Taifa langu inafuzu michuano mikubwa kabisa barani Africa na michuano maarufu pia Duniani.
March 24 ni siku ambayo nitawasimulia watoto na wajukuu zangu kilichotokea pale Kwa Mkapa huku nikishuhudia kwa macho yangu na nikiwa miongoni mwa Watanzania walioifikia hii ndoto.
Nikiwa katika uwanja kama “Website Reporter” wa Kandanda.co.tz ni mechi pekee ambayo nilifanya kazi na kuondoka na furaha zaidi katika uwanja wa Taifa kuliko zote nilizowahi kuhudhuria na kuripoti.
March 24 itabaki kua ni siku kuu ya furaha katika maisha yangu ya soka.