Sambaza....

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza neema kwa Timu yetu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” endapo itakata tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon. 

Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast mapema mwakani kati ya January na Februari 2024. Na Stars ipo kundi F pamoja na Uganda, Algeria na Niger katika kufuzu michuano hiyo.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dr Pindi Chana amesema serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni 500 endapo Taifa Stars itafuzu michuano hiyo ya Afcon 2023.

Stars ipo kundi F ikiwa na alama moja pekee baada kucheza michezo miwili wakifungwa na Algeria na kupata sare dhidi ya Niger ugenini na hivyo kushika nafasi ya mwisho katika kundi hilo.

Simon Msuva na wenzake tayari wapo Misri wakijiandaa na mchezo huo dhidi ya Uganda

Sasa Stars wana kibarua kigumu dhidi ya majirani zetu Uganda ambapo kutakua na michezo miwili ndani ya siku nne. Stars itaanzia ugenini Machi 24 nchini Misri kabla ya kurudiana tena Machi 28 nyumbani.

Tayari Shirikisho la Soka nchini TFF limetangaza viingilio kuelekea mchezo huo wa nyumbani utakaopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa. VIP A ni 10,000, VIP B ni 5000 na mzunguko ni 3000. 


Sambaza....