- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
The worst Under 17 Team nimewahi iona hapa Tanzania toka mwaka 2010 labda. Last time nilisema hapa kuwa square passes at the defending zone are uncountable! Watoto wanaona raha tu kupiga pasi kushoto kulia kushoto kulia kama gwaride.
Mpira ukisogea katikati, anayeuchukua anawaza kupiga mpira mrefu tu pembeni kwa Kevin John ili akimbie nao mpaka kwenye box. Halafu Kelvin (Kelvin John) anapokimbia, timu yote imebaki chini, yuko peke yake dhidi ya wapinzani watano.
Timu haiwezi kutembea na mpira! Watoto hawajiamini kabisa wanapiga mipasi ya hovyo mingi sana.
Overall, timu ni kama haikuandaliwa kwa sababu hakuna muunganiko wa idara, kutoka ulinzi kiungo mpaka mbele hauonekani muunganiko.
Kipa anacheza peke yake, defenders are doing the same na strikers wanakimbia peke yao huku midfielders wakiwa wamesimama katikati ya uwanja utadhani wanacheza halaiki ya kuzima mwenge!
Fedrick Jailos!, #KandandaChat