BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, Seleman Kidunda leo ameingia mkataba wa pambano na Kampuni ya mchezo wa ngumi za kulipwa PAF Promotion Entertainment Company linalotarajia kupigwa Juni 30, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Kidunda ameingia mkataba huo kwa ajili ya pambano hilo atakalocheza dhidi ya Eric Mukadi raia wa DR Congo anayeishi Afrika Kusini huku Mfaume Mfaume akitarajia kucheza na Nkululeko Mhlongo raia wa Afrika Kusini.
Akizungumza mara baada ya kusainisha mkataba, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Fadhili Maogola alisema wameamua kumchukua Kidunda katika pambano hilo kutokana na kutambua ubora wake huku wakiamini ataotoa upinzani wa kutosha kwa mpinzani wake kutoka Afrika Kusini licha ya kuwa na uraia wa DR Congo.
“Tumempa mkataba, Kidunda kwa ajili ya pambano letu la hata usipo lala pata kucha, yeye na Mfaume watapanda katika ulingo mmoja siku hiyo pale Mlimani City kuonyesha ukali wao katika mapambano ambayo yatakuwa yakimtaifa, hakuna asiyejua ubora na wake.
“Lakini siyo Kidunda peke yake wapo na wakali wengine ambao watapanda ulingoni kuonyesha ufundi wa mchezo wa ngumi, raia yetu bado tunaomba wapinzani wajitokeze kwa wingi kuhakikisha tunalipa hadhi pambano letu, ” alisema Maogola.
Kwa upande wa Kidunda alisema kuwa Kidunda alisema kuwa: “Kwanza nashukuru kwa kuweza kupata hili pambano kwa sababu mara ya mwisho nilipanda ulingoni kule Songea katika pambano langu la Katompa, mashabiki wangu nataka kuwaambia narudi tena kwa moto, mkubwa maana siku zote mimi sipigani ila nacheza ngumi, “.