Klabu ya soka ya KRC Genk anayocheza mtanzania Mbwana Ally Samatta imepangwa kucheza na Slavia Prague ya Jamhuri ya Cheki katika hatua ya 32 ya michuano ya Europa Ligi.
Genk ambayo ilimaliza kinara wa kundi I ambalo lilikuwa na timu ngumu kama Malmo na Beskitas imepangwa kukutana na miamba hiyo ya Cheki ambao wao walimaliza nafasi ya pili nyuma ya Zenit St. Petersburg katika kundi C.
Genk wataanzia Ugenini katika uwanja wa Eden Arena kabla ya kurudiana baadae kwenye uwanja wa nyumbani wa Genk Cristal Arena.
Samatta mpaka sasa ana mabao matatu katika dakika 426 alizocheza pamoja na kuchangia bao moja katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya.
Europa League hatua ya 32 droo
Viktoria Plzen v Dinamo Zagreb
Club Brugge v Red Bull Salzburg
Rapid Vienna v Inter Milan
Slavia Prague v Genk
Krasnodar v Bayer Leverkusen
FC Zurich v Napoli
Malmo v Chelsea
Shakhtar Donetsk v Eintracht Frankfurt
Celtic v Valencia
Rennes v Real Betis
Olympiakos v Dinamo Kiev
Lazio v Sevilla
Fenerbache v Zenit St Petersburg
Sporting Lisbon v Villarreal
Bate Borisov v Arsenal
Galatasaray v Benfica