Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu kutoka Al Hil ya Sudan wameshawasili Tanzania asubuhi hii tayari kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa.
Tanzania itacheza na Uganda katika mchezo muhimu wa kutafuta tiketi ya AFCON.