Sambaza....

Mshambuliaji kipenzi wa Simba Pape Osmane Sakho ni kama ameanza kuaga hivi katika viunga vya Wekundu wa Msimbazi Simba baada yakuweka picha yenye kuashiria kuaga katika ukurasa wake wa instagram.

Sakho mpaka sasa amefunga mabao 6 na kutoa pasi 5 za mabao katika michezo ya Ligi Kuu pekee na pia alifunga mabao matatu katika michuano ya Kimataifa.

Picha aliyoiweka katika ukurasa wake wa instagram Pape Osmane Sakho.

Msemaji wa Simba Ahmed Ally alikiri mwanzoni mwa mwaka huu walipokea ofa nono kutoka klabu ya Al-Hilal ya Sudan wakimuhitaji Msenegali huyo mwenye msimu mmoja tuu na klabu ya Simba.

Sakho amejiunga na Simba akitokea klabu ya Teungeuth Fc ya nchini kwao Senegeal alipotoka kua mchezaji bora wa msimu.

Sambaza....