- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Afisa habari wa Lipuli FC , bwana Clement Sanga amesema kuwa mwisho wa Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho ni kwenye uwanja wa Samora.
Akizungumza na mtandao huu wa Kandanda.co.tz amedai kuwa kuna watu wanadai Lipuli walibahatisha kuifunga Yanga katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Lipuli waliifunga Yanga kwa goli moja kwa bila katika uwanja wa Samora. Na lipuli wamefanikiwa kuingia katika hatua ya nusu ya fainali ya kombe la shirikisho baada ya kuifunga Singinda United.
Yanga na Lipuli watakutana katika hatua ya nusu fainali baada ya Yanga kuitoa Alliance Schools kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Mchezo mwingine wa nusu fainali katika kombe hili la shirikisho itawakutanisha KMC na Azam FC. Azam FC waliitoa Kagera Sugar kwa goli moja kwa bila na KMC waliwatoa mabingwa watetezi Mtibwa Sugar.