Mshambuliaji wa zamani wa Tp Mazembe ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) amevunja rasmi mkataba wake na klabu ya Al Hilal ya Sudan.
Imeripotiwa Mshambuliaji Thomas Ulimwengu amevunja mkabata wake na klabu ya Al Hilal ya Sudan akiwa amedumu kwa miezi mitano tu.
Kabla ya kwenda Al Hilal ya Sudan, Iliripotiwa Thomas Ulimwengu kujiunga katika klabu ya Yanga ya Dar es Salaam. Kuvunja kwake mkataba kunaweza kumpa nafasi kubwa yeye kujiunga na klabu hii ambayo aliripotiwa kujiunga nayo awali.