Sambaza....

Droo ya robo fainali ya Ligi ya Soka ya Afrika ilifanyika mjini Cairo Jumamosi na imewakutanisha Simba Sc dhidi ya Al Ahly ya Misri katika robo fainali.

Ligi ya Soka ya Afrika ni jina jipya la kile kilichotangazwa hapo awali kama CAF African Super League, ambayo itaendelea kati ya 20 Oktoba na 11 Novemba 2023 na mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utafanyika nchini Tanzania utawakutanisha Simba na Ahly.

 

Hii ndio litakua ni tolea lakwanza la michuano hiyo, litakuwa shindano la mtoano kutoka robo fainali hadi nusu fainali na fainali, kulingana na mechi za nyumbani na ugenini.

Ni michuano ambayo kwa kiasi kikubwa itawanufaisha vilabu shiriki kiuchumi. Mshindi wa michuano hiyo atapata dola milioni 11 na kila timu itapewa dola 2.5 kwaajili ya maandalizi ya michuano hiyo.

Mamelodi Sundowns itacheza dhidi ya Petro de Luanda katika droo hiyo na mshindi kati yao ndio atacheza na Simba SC au Al Ahly katika nusu fainali.

Wakati katika upande wa pili Enyimba atamenyana na Wydad Casablanca na mshindi atakutana na TP Mazembe ama Esperance de Tunis.

Kwa upande wa Simba hii ni nafasi nyingine yakuandika historia katika michuano hii mipya ya vigogo wa Afrika. Licha ya kuonekana wakifanya vyema katika michuano ya Afrika lakini mara kwa mara wamekua wakiishia robo fainali na hawakuwahi kukaribia kuvaa hata medali.

Tayari hata kabla msimu haujaanza walishajiandaa vyema wakifanya usajili na kuweka kambi nzuri nje ya nchi kujiandaa na michuano hiyo iliyokua inajulikana kama Super League hapo awali.

Sambaza....