Sambaza....

Wapwa Sadio Kanuote “Putin” alikosa michezo yote miwili ya Simba dhdi ya Raja Casablanca katika hatua ya makundi lakini sasa atacheza mchezo wa marudiano ugenini kati ya Simba dhidi ya Wydad Cadablanca baada ya kucheza ule wa awali wa hapa nyumbani.

Benchi la ufundi la Simba likamwandae vyema Sadio Kanoute kuepuka kadi kuelekea kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Wydad Casablanca ugenini nhini Morocco katika uwanja mgumu wa Mohamed V.

Kanoute ni ”harsh midfield” kwenye aina ya viungo waliopo katika kandanda kwasasa hana masihara wala mzaha hata kidogo akiwa eneo lake.

Kuna imani kwamba ukicheza idara ya kiungo maisha ya kadi za njano na nyekundu ni ya kawaida, haswa eneo la kiungo mkabaji.

Sadio Kanoute (kulia) akianua mpira mbele ya mshambuliaji wa Wydad Casablanca.

Kuna chembechembe za ukweli na za kubuni ndani yake kuna wachezaji wamecheza idara hiyo kwa miaka kadhaa lakini hadi wanamaliza uchezaji  wao hawaijui kadi nyekundu ni kitu gani.

Putin kama wanavyomuita huyu ni Mzee wa miba anaumisha sana watu nge’ na ndiyo maana kukuta amesimamishwa mchezo si jambo la kushangaza kabisa.

Nakwenda kumuangalia umuhimu wake kwenye mechi ijayo nakiri uwepo wake unafaida kubwa sana kwa Simba haswa kutokana na mazingira ya mchezo.

Natoa angalizo la kuwa makini kwenye suala la kadi kwakuwa  kwa sayansi ya mchezo inataka kujua tabia ya wapinzani unaokabiliana nao iwe hasi ama ni chanya kwa mchezaji moja moja na timu yote kiujumla.

Sadio Kanoute “Putin” akimuacha chini kiungo wa Yanga Khalid Aucho katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Hapa ndiyo nafasi ya “Video analysist” wa timu inapokuja, najua mpira  wa Africa unachezwa kwa mbinu zaidi na fitna  za Kidunia za nje ya Uwanja. Kunauwezekana timu kupunguziwa uzito wa mchezo kwa kutumia kadi hii imetokea mara nyingi tu.

Hivyo basi kwa aina  ya uchezaji wa mshikaji wangu Putin nimeweka kama angalizo na hasa ukichukulia viungo wenzake atakaokutana nao upande wa Wydad hawagongani akina Yahaya Jabrane, Daoudi na Ayman el Hassoun.

Huku kwa upande wa Simba kutakuwa na punda mwingine Muzamir Yassin katika kiungo pamoja na kina Kibu Denis, Clatous Chama na Ntibazonkiza Saidoo kifupi nionavyo mimi  kutachafuka kwenye eneo la kiungo.

Sambaza....