Sambaza....

Sadala Mohamed Lipangile au unaweza kumuita Sadioo amekua katika wakati mzuri wa kuweza kufumania nyavu na kuwatesa makipa wa timu pinzani huku akiwa katika nafasi nzuri ya kua Galacha wa mabao kwa mwezi January.

Sadala amekua msaada mkubwa kwa klabu yake ya KMC baada ya kuanza kuonyesha nuru kwenye ufungaji. Kiasili Sadala Lipangile ni mlinzi wa kati lakini huwa anatumika kama mshambuliaji wa kati pia na huonyesha kumudu nafasi hiyo na kuitendea haki.

Sadala Lipangile katika mchezo dhidi ya Coastal Union!

Kutokana na hali ya majeruhi kuwakumba washambuliaji wa KMC (Salim Aiyee, James Msuva, Charles Illanfia na Cliff  Biyoya) Sadala amekua akitumika kama mshambuliaji na kuweza kufanya kikamilifu kazi ya kuweka kambani.

Na.MchezajiTimuNafasi
1rwaMeddie KagereMshambuliaji62
2tanJohn R. BoccoMshambuliaji44
3tanFeisal SalumKiungo39
4bdiSaid NtibazonkizaKiungo36
5codFiston MayeleMshambuliaji33

Mpaka sasa Sadala amefunga magoli sita na “assist” moja katika michezo minne ya hivi karibuni.  Sadala Lipangile amefunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya  Singida United ugenini, pia amefunga mabao mawili dhidi ya mabingwa wa Mapinduzi Mtibwa na Sugar na pia magoli mawili dhidi ya Pan Africa katika michuano ya FA.

Sadala Lipangile “Sadio”

Katika chati ya ufungaji bora wa mwezi January Sadala Lipangile yupo kileleni akiwa na magoli manne na hivyo kumfanya kukaribia kuwa Galacha wa magoli kwa mwezi huu.

Je Sadala Lipangile tumaini jipya kwa mwalimu Ettiene Ndayiragije katika kusuka kikosi kwaajili ya michuano ya CHAN?

 

Sambaza....