Galacha wa Mabao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kelvin Sabato, amekabidhiwa kiatu chake baada ya kuibuka galacha kwa kufunga mabao matano mwezi Februari mwaka huu. Mtandao wetu husheherekea na wafungaji bora wa kila mwezi wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Sabato aliifungia klabu yake ya Kagera Sugar mabao matano, moja akiifunga Mwadui FC, Matatu Singida United na goli moja akiifunga Tanzania Prisons. Hadi sasa ameshafunga mabao 6 katika ligi hii, akiisaidia Kagera Sugar kufanya vizuri katika Ligi Kuu.
Kelvin akiongea na mtandao huu wakati akikabidhiwa zawadi zake ambazo zimedhaminiwa na Mgahawa Cafe & Restaurant, alisema ni Abdallah Mfuko ambaye ni beki wake bora zaidi tulipotaka kujua ni maoni yake kuhusu beki gani mgumu.
“Mfuko anatumia akili sana na pia yuko sawa kimwili” Kelvin Sabato. Mfuko ambaye amewahi kuzichezea Ndanda na Mwadui, kwa sasa anachezea klabu ya KMC FC. Katika mchezo uliopita Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya KMC.
Mtandao wetu unaendelea kusheherekea na wafungaji wa mabao kila mwezi, na tayari mwezi huu huenda tukasheherekea na Meddie Kagere ambaye tayari ameshafikisha mabao matano hadi ligi iliposimama.