Klabu ya Real Madrid inashikilia rekodi ya kutwaa taji la Ligi ya mabingwa Ulaya mara tano mtawalia, hii ilikua toka mwaka 1956 mpaka 1960.
Katika miaka mitano hiyo Madrid walikua moto wa kuotea mbali kiasi kwamba kupelekea kuogopwa sana barani Ulaya na hivyo kupelekea kuwa mabingwa wa muda wote wa kombe hilo mpaka sasa. Real Madrid ina jumla ya makombe 14 ya Ligi ya mabingwa Ulaya kabatini mwake.