Sambaza....

Mwaka 1967 klabu ya Celtic (Lisbon Lion) ilishinda ubingwa wa Ulaya ikiwa na wachezaji wazawa ambao wamelelewa katika viunga vya Dimba lao la nyumbani yaani Celtic Park.

Walishinda ubingwa wa Ulaya kwa kuwafunga Inter Milan mabao mawili kwa moja kwenye Dimba la Estadio Nocional. Kikosi hicho kilikua na wachezaji 15 na 14 kati yao walitokea (asili) maili 10 kutoka ulipo uwanja na mmoja pekee alitoka maili 20 kutoka hapo.

Msimu huo Celtic walitawala mashindano ya Ulaya na kujulikana kama “Expansive Team” yaani timu inayocheza kwa kujitanua uwanjani huku wakiwa na kasi kubwa huku hayo yakichagizwa na wachezaji hao kucheza kwa morali ya juu.


Sambaza....