Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la soka nchini (TFF), limetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa makamu wa raisi wa Shirikisho hilo Michael Wambura aliyepinga kufungiwa maisha.
Wambura alifungiwa maisha na kamati ya maadili kufuatia kufunguliwa mashitaka na Sekretarieti ya TFF.
Mwenyekiti wa kamati ya rufani, ndugu Ebenezer Mshana, ameviambia vyombo vya habari kuwa baada ya kusikiliza na kuchanganua hoja za pande zote mbili waliona kuwa Wambua amekutwa na hatia.
“Baada ya kusikiliza rufani zote za Wambura tumeona kuwa Wambura alikuwa na makosa, na tunaiomba Sekretarieti ya TFF iende mbali zaidi katika kesi hii” alisema Ebenezer.
Naye Wakili anayemtetea Wambura, Emmanuel Muga, alisema kuwa mteja wake alishajuwa kwamba hayo ndiyo yatayotokea baada ya kamati kubadilishwa .
” Wambura aliniambia kuwa kikao kikimalizika niongee na nyinyi, kwa sababu alijua kitu ambacho kitatokea, lakini tutakata rufaa na kwenda mbele zaidi”.
Aidha Wakili huyo aliongeza kuwa alishangaazwa na Mwenyekiti huyo kusoma upande wa TFF, kuwa aliomba mteja wake apunguziwe adhabu na iwe ni ya miaka mitano badala kufungiwa maisha.
“Kama ningekuwa nimesema hayo basi ingesomwa kunako utetezi wetu lakini haikusemwa hili ni jambo linalostua, tutakata rufaa na kwenda mbele zaidi” alisema Muga.
Pia rufaa zingine zilisomwa na Ebenezer, rufani ya kiongozi wa Ndanda FC Dustan Mkundi ambaye kesi yake kamati imeiamuru TFF, kupeleka suala lake kunako vyombo vya uchaguzi.
Rufani nyingi ni ya Edgar Chibula, kiongozi wa Abajalo FC ambaye alitoa lugha chafu kufuatia kuahairishwa kwa mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons, lakini aliomba msamaha kwa kamati na kukiri makosa yake hivyo amesamehewa