Sambaza....

Wachezaji nyota Ulimwenguni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanarejea kuzitumikia timu zao za Taifa kwa mara ya kwanza toka kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia iliyomalizika mwaka jana nchini Russia.

Messi anatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa leo Ijumaa ambapo Argentina watacheza dhidi ya Venezuela jijini Madrid kwenye mchuano wa kirafiki wakati Ronaldo yeye atakuwa na kikosi cha Ureno kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Ukraine jijini Lisbon.

Mapacha hawa kwa pamoja wamekosa michezo sita kwenye timu zao Taifa, ambapo Ureno walifika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya National League bila ya kuwa na Ronaldo, hata hivyo staa huyo mwenye umri wa miaka 34 akicheza michezo 154 na kufunga mabao 85 anatarajiwa kuwepo tena kwenye mchezo wa Machi 25 dhidi ya Serbia.

http://www.kandanda.co.tz/morocco-vs-argentina-mkataba-wa-ajabu-wa-kumlinda-messi/

Wakati Messi mwenye umri wa miaka 31 ameshafunga mabao 65 kwenye michezo 128 aliyocheza na timu ya Taifa anarudi kwenye kikosi hicho huku wachezaji wengine kama Sergio Aguero, Gonzalo Huguain na Mauri Icardi wakikosekana kwenye kikosi cha Argentina.

Sambaza....