Sambaza....

Mshambuliaji wa zamani wa PSG, Fulham na Manchester United Luis Saha amewataja wachezaji wake bora duniani kwasasa akiwataja nyota wawili kutoka Ufaransa na Uingereza.

Raia huyo wa Ufaransa amewataja Kylian Mbappe kutoka PSG na Marcus Rashford wa Manchester United kama wachezaji bora duniani kwasasa. Wawili hao kwa pamoja wamefunga mabao 31 kwa pamoja, Mbappe (15) na Rashford (16).

“Hakuna wachezaji bora kuliko Rashford kwa sasa kwenye soka la dunia, lakini Kylian Mbappe bado ni bora kwani amekuwa mzuri zaidi kwa miaka mitatu iliyopita na bosi wa PSG, hata akiwa pamoja na kina Neymar na Lionel Messi huko,” Saha aliliambia Daily Post alipokua akifanya mahojiano na Lord Ping.

Luis Saha pia aliongeza “Erling Haaland anacheza vizuri, lakini hana manufaa zaidi. Matamanio, kasi, na kujiamini kwa kijana huyu kwa sasa (Rashford), huwezi kucheza nae na Kylian Mbappe ni sawa. Haiwezekani kuwazuia wachezaji hawa mahiri.”

Marcus Rashford.

Marcus Rashford anatarajiwa kuiongoz United walau kupata kikombe cha kwanza tangu waliponyakua kombe wakiwa chini ya Jose Mourinho watakapokua uwanjani Wembley Jumapili  dhidi ya Newcastle United katika fainali ya Carabao Cup.

Tangu kumalizika kwa kombe la Dunia nchini Qatar Marcus Rashford amerudi katika klabu yake akiwa na kasi ya ufungaji huku akiwa ndie mchezaji aliefunga mabao mengi zaidi baada ya Kombe la Dunia kwenye Ligi zote  kubwa barani Ulaya.

Kylian Mbappe na Neymar Junior.

Kwa upande wa Mbappe ameendelea kufanya alichokifanya tangu alipoanza msimu huu na PSG na hata timu ya Taifa ya Ufaransa katika Kombe la Dunia mpaka hatua ya fainali.

Sambaza....