Sambaza....

Imeripotiwa kuwa klabu ya soka ya AS Roma ya nchini Italy ipo mbioni kumtangaza kocha aliyetimuliwa hivi majuzi kunako klabu ya Fulham ya England Claudio Ranieri kama kocha wao mpya.

Roma ambao waliachana na kocha wao Eusebio Di Francesco baada ya kuondolewa kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Porto ya Ureno siku ya Jumanne.

Miongoni mwa majina ambayo yamependekezwa kwa ajili kuchukua nafasi ya Eusebio Di Francesco ni kocha Ranieri ambaye naye alitimuliwa juma lililopita baada ya kuandikisha matokeo mabovu akiwa na Fulham.

Ranieri anatarajiwa kusafiri kuelekea jijini Roma mwishoni mwa juma ili kuzungumza vipengele vya mkataba kabla ya kusaini mkataba na miamba hiyo ya soka nchini Italy.

Ranieri alishawahi kuifundisha Roma kati ya mwaka 2009 na 2001 na kuisaidia kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi mwaka 2010, na anafahamika zaidi baada ya kuiongoza Leicester City kutwaa ubingwa wa England mwaka 2016.

Sambaza....