Golikipa namba tatu wa klabu ya Yanga , Ramadhani Kabwili ambaye alikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha , amepata majeraha mengine tena baada ya kufanikiwa kupona majeraha ya awali.
Ramadhani Kabwili amepata majeraha mapya baada ya kupata ajali ya bodaboda , ajali ambayo imesababisha yeye kupata majeraha sehemu ya uso.
“Amepata majeraha ya bodaboda , kwa sasa sehemu yake ya uso ana majeraha makubwa ambayo yamesababisha yeye kama yeye asiendelee kuwepo kwenye sehemu cha kikosi ambacho kitaanza mazoezi kwa ajili ya ligi kuu Tanzania bara” alisema daktari wa Yanga
Bwana Ngazija ambaye ni daktari mkuu wa Yanga amedai kuwa wamempima Ramadhani Kwambili na wamegundua kuwa anaendelea vizuri ila kwa sasa ana makovu peke yake.
“Tulienda kumpima kwenye X-Ray tumegundua hajaumia sana , licha kwa sasa kuwa na makovu peke yake. Anaendelea vizuri ingawa hatokuwa sehemu ya kikosi cha Yanga SC kitakachoanza mazoezi”- alisema daktari huyo wa Yanga SC