Raisi wa klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Said amezungumzia sakata la timu yake ya Yanga na kiungo wao Feisal Salum leo alipokua akizingumza katika kipindi cha asubuhi cha Clouds Fc.
Pamoja na kuongelea mambo kadhaa kuelekea katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika pia Injinia Hersi Said amezingimzia uelekea wa nyota na nahodha wao kutoka Zanzibar. “Feisal ni mmoja kati ya Wachezaji bora na wenye nidhamu ambao tumewahi kuwa nao Yanga hadi leo katika wachezaji ambao niliwakuta Yanga, yeye ni mchezaji mkongwe zaidi kati ya wote sababu hakuna yeyote aliyesalia Yanga hadi leo ispokuwa yeye,” alisema na kuongeza injinia Hersi Said
“Lakini pia hajawahi kuwa na changamoto yoyote ya kinidhamu, alikuja akiwa mdogo ndio maana akapewa jina la Fei Toto.”
Hersi pia aligusia katika swala la maslahi ya mchezaji huyo wa Zanzibar Heroes na kusema wao ndio waliokua wakwanza kuona thamani yake na kuamua kumboreshea mkataba wake
“Kama GSM tuliwahi kumwita Feisal na kukaanae kujadili maslahi yake ambayo hayakuwa madogo hata kwa wakati huo, alikuwa akipokea mshahara wa Tsh 1.5m na tukamuongezea hadi kufikia Tsh Million 4 kwa mwezi pamoja na signing fee ya Tsh Million 100, kuna Watu wanauliza kuhusu maslahi ya Feisal ikiwa sisi tuliyaboresha tangu mwaka 2020”
“Sitaki kwenda mbali ila mimi naamini kuna kitu nyuma ya Feisal kinachomsukuma kufanya haya” alisema Rais Hersi Said.
Rais huyo wa Yanga pia hakua na shida na Feisal na kusema wamempa machaguo ambayo yeye mwenyewe ataamua alifuate lipi ili aweze kuendelea kucheza soka.
Hersi Said “Fei tumempa machaguo matatu, mosi arudi aje amalizie mkataba wake, pili aje aboreshe maslahi yake maana nafasi ipo bado na tatu timu inayomtaka ije tuzungumze mezani.”
Mara ya mwisho Feisal alionekana akiwa Zanzibar pamoja na kiungo wa Simba Sc Clatous Chama wakila raha katika fukwe za Zanzibar.