Sambaza....

Bujumbura hadi Dar-es-salam ni umbali takribani kilomita 1,500 kwa basi, hivyo unapozungumzia kwenda na kurudi, unazungumzia takriban kilomita 3,000 hivi, hivyo utakubaliana nami si karibu,  ni mbali hasa.

Sasa ngoja nikupe “Raha ya goli la Mbali” ukiachilia uchovu huo wa safari ndefu. Siku zote “mtembea bure si sawa na mkaa bure” na hapa tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kwenda salama na kurejea salama.

Mpwa wenu Tigana, nikiwa Burundi

Mpwa wenu ukiachilia mbali Uwanahabari wangu , huwa naingia kwenye engle nyingine ya kiufundi katika soka. Pamoja na kwamba nilijua mahitaji ya mechi ya ugenini kwa Taifa Stars, hasa unapozungumzia mechi za mtoano (knockout stage) huwa zina ufundi na tamaduni zake jinsi ya kucheza.

Ukumbuke mechi hii ni ya kuwania kufuzu kombe la dunia ambapo nafasi huwa ni finyu sana.  Ikiwa na maana ya kwamba mataifa 54 toka CAF yanagombea nafasi 5 za kuwakilisha katik fainali ya kombe la dunia Qatar 2022. Kwa mataifa 54 kugombea nafasi 5 ni wastani wa kila mataifa 11 yanagombea nafasi 1. Nini namaananisha hapa Wapwa zangu, ni “ufinyu” wa nafasi hizo, pressure ya kuzipata na pupa na papara.

Hivyo basi unapocheza mechi hizi hasa katika hatua ya mwanzo ya mtoano, hutakiwi kumburudisha mtu, unatakiwa kufocus kwanza kufuzu kwa kuwa hakuna wasaa wa kijiuliza Mara mbili mbili.

Tofauri kabisa na hatua ya makundi game strategic ni tofauti, inakupa nafasi ya kuandaa ramani yako ya vita vizuri ikiwemo kupoteza baadhi ya mechi na kujiuliza tena.

Kwenye “Raha ya Goli la mbali” kwa kisa cha safari ya burundi ni kwamba Game plan ya kwanza (dhamira )
1 Kushinda mchezo kwa sababu tutajiweka mazingira mazuri ya asilimia 75% kufuzu

2 Kusare au kusuluhu , Kwa maana ya kupata point 1 na kuifanya 50% ya kufuzu

3 Ni kupata goli lolote katika mchezo wa ugenini kama stepping stone katika mchezo wa ugenini.

Msanii Kakaman aliwahi kuimba wimbo wa Aisha wenye kibwagizo ndani yake “raha ya mechi bao” . Japo sina uhakika alimaananisha kile ninacho kimaananisha mimi achana na hilo Wapwa zangu!

Kwenye Mchezo ule wa Burundi pale Stade Intwari, wakiwa na maana wa “uwanja wa mashujaa” nami nilikuwa shujaa kwa “kuanikiaza”.  Ushindi mwanzo mwisho na Simon Msuva na Watanzania wote tuliokuwepo uwanjani tukawa mashujaa. Mpwa ukitaka kujua kwanini tulikuwa mashujaa ni the way tulivyowajibika kila moja katika eneo lake, Wachezaji, Makocha, Shabiki na Wanahabari.

Waandishi wa Habari waliokuwa wameongezana na Taifa Stars wakiwa Dodoma, njiani kurudi Dar

Binafsi Mpwa wenu nahitimisha kwa kusema tumetoka sare ya  1-1 na tumepata faida kuu 3:
1 Tumepata Pointi moja
2 Tumefunga goli ugenini
3 Tumeingiza mchezaji kwenye orodha ya wafunga akiwa na wastani wa goli 1 mechi 1

Faida yake nini Wapwa zangu? Tumeweka ugumu kwa mpinzani kunufaika na goli la ugenini, mpaka apate sare ya juu ya goli 2 kinyume na hapo ni kwenye eneo la kushinda tu.

Mimi niseme “Raha ya goli la mbali “( ugenini) ni hiyo. Nini cha kufanya kwa upande wa benchi la ufundi? …ni kumalizia “robo duara”.

Mpwa wenu nawapa Taifa stars 75% kufuzu makundi, ila tujitokeze kwa wingi “kuanikiza” ushindi siku ya Jumapili.

#fyekaburunditusonge

Sambaza....