Mpira ukamalizika kwa 2-0
Samata anatokacanaingia Mandawa
Dakika 5 zimeongezwa
Mpira unaendelea bado matokeo ni yaleyale, dakika ya 44 kipindi cha pili
Mbwana Samatta ametolewa nje kwa maumivu, anatibiwa.
Mpira burudani kabisa hapa uwanja wa Taifa, Amunike anajionnyesga utaalamu wake, Mashabiki hapa wanatamani Mkude angekuwepo… hata hivyo Fei Toto, Nyoni,Himid Mao burudani ya kutosha pia.
TANZANIA 2- 0 CAPE VERDE
Msuva (Samatta), Samatta (Mudathir)
Dakika ya 58, Mbwana Samatta anafuta dhambi zake zote na kufunga bao la pili assist kutoka kwa Mudathir Yahya. #TupoPamojaTaifaStars
Abdi Banda ametoka, John Bocco ameingia dakika ya 7 kipindi cha pili.
Mashambulizi kadhaa kuelekea Cape Verde, lakini pia wao pia wanashambulia pia
Mpira umeanza kupindi cha pili
Mpira ni Mapumziko sasa, baada ya dakika 2 kuongezwa katika kipindi cha kwanza.
Mpira ilibidi kusimama kwa muda kupisha Aishi Manula apatiwe matibabu uwanjani.
Cape Verde pia wananafannya mashambulizi hatari langoni mwa Tanzania, lakini uimara wa Aishi na Kamati yake ya ulinzi ikiongozwa na Yondani, Morris, kapombe na Banda.
Samatta, aliambaa na mpira winga ya kulia na kuingiza vizuri mpira katika kumi na nane, Simon Msuva akashindwa kutumia nafasi hii, na kuupiga nje ya goli.
@msuva anaipatia Tanzania bao la kwanza dakika ya 28, kazi nzuri kutoka kwa @samatta77 #TupoPamojaTaifaStars
Mbwana Samatta amekosa penati iliyopatikana dakika ya 21. Ilisababiahwa na Simon Msuva.
Penati imegonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani.