Sambaza....

Beki wa kati aliyestaafu wa Afrika Kusini, Lucas Radebe alikaa miaka mitano Kaizer Chiefs kabla ya kujiunga na Leeds United mwaka 1994. Awali alikuwa golikipa, alibadili nafasi na kuwa kiungo wa kati na kisha nafasi ya ulinzi ya kati.

Leeds ilimsajili raia mwenzake Phil Masinga pamoja na Radebe. Leeds waliripotiwa kuvutiwa zaidi na Masinga na Radebe alijumuishwa tu kwenye mpango huo ili kumfanya Masinga asiwe mpweke. Lakini mwishowe, Radebe ndiye aliyekuja kuwa bora zaidi pale Elland Road.

Lucas Radebe.


AkiwaLeeds, Radebe alicheza katika nafasi ya golikipa mara kadhaa, kwenye mechi dhidi ya Middlesbrough Machi mwaka 1996 wakati kipa John Lukic alipojeruhiwa na kwenye mechi dhidi ya Manchester United wakati kipa Mark Beeney alipotolewa nje kwa kadi nyekundu.

Radebe aliteuliwa kuwa nahodha wa Leeds msimu wa mwaka 1998-99. Alipokuwa nahodha, Leeds walimaliza katika nafasi ya 4 kwenye Premier League msimu wa mwaka 1998-99, walimaliza nafasi ya 3 msimu wa mwaka 1999-2000 na walifika nusu fainali ya UCL mnamo msimu wa mwaka 2000-2001. Kwa jumla, aliitumia miaka 11 huko Leeds.

katika ngazi ya kimataifa, aliichezea Afrika Kusini mara 70 na alikuwa mmoja wa wachezaji karika kikosi kilichoshinda AFCON mwaka 1996. Pia aliwahi kuwa nahodha wa Afrika Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 1998 na mwaka 2002.


Sambaza....