- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
- Yanga na Rekodi iliyoshindikana
- Ratiba ya Mechi zote Ligi Kuu Tanzania
Taarifa za kifo cha Ibrahim Rajabu el maarufu ”JEBA” nimezipokea kwa huzuni sana, kiungo aliyekuwa na ufundi mkubwa wa mpira asiye na tabasamu usoni japo ufundi wake ulilete tabasamu kwa walio wengi.
Wengi tulimfahamu akiwa kwenye kilele cha ubora wake wa kiuchezaji pale Mtibwa, akitengeneza combinationa na nyota kadhaa, Jeba pia amewahi ichezea Azam Fc.
Mengi yanaelezwa juu ya afya yake lakini hakuna anayeweza kuthibitisha juu ya tatizo alilokuwa nalo kabla ya umauti wake.
Ninachoweza kusema ni kuwa tumeondokewa na mchezaji bora wa wakati wake, ambapo kutokana na kukosa tabasamu uwanjani wengi waliamini anapania mechi kumbe ile ndiyo aina yake ya uchezaji (play style yake).
Hakuwa na umbo kubwa ila alitambua, kutatua tatizo la umbo lake dogo ni kucheza kwa akili na maarifa ya hali ya juu. Speed yake yakuvutia uwezo wake wa kugeuka na mipira kukusanya kijiji kama si kata nzima hakika alikuwa kiungo bora ambaye macho hayawezi kukinai kumuangalia.
Aling’ara sana katika michuano ya Mapinduzi Cup pamoja na ligi nzima ya Tanzania bara.
Inna lilah wa inalilah rajiun kiungo fundi wasoka unayefariki siku Moja na kiungo mwenzako wa zamani wa Uholanzi na klabu ya Rangers ya Scotland, Fernando Ricksen