Walianza wao kufunga goli kipindi cha kwanza , goli ambalo liliwapa nguvu kubwa sana ya kutawala mchezo wa jana kwa dakika nyingi , Lakini dakika 5 za mwishoni zilileta maumivu na machozi.
Maumivu ambayo yaliletwa na Ibrahim Ajib , Ibrahim Ajib ambaye aliingia kipindi cha pili na miguu yake ikafanya kazi ya kutoa pasi ya mwisho ya goli pamoja na kufunga goli la ushindi.
Baada ya mchezo huo nilimuuliza kocha mkuu wa Polisi Tanzania , Malale Hamsini kwanini hawakutumia vyumba vya kubadilishia nguo vya kubadilishia nguo alidai kuwa walizimiwa umeme.
“Chumba chetu kilikuwa kimezimwa umeme , mpaka sasa hivi sijui sababu ni nini ndiyo maana tuliamua kutumia chumba hiki cha kufanyia mikutano na waandishi wa habari kama chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko “alisema kocha huyo.
Lakini nilizidi kufanya udadisi zaidi nilienda kumuuliza mmoja ya viongozi wa timu ya Polisi Tanzania ambaye aliniambia kuwa kulikuwa na dawa kwenye chumba chao.
“Chumba chetu kilikuwa na hewa nzito , hewa ambayo ni kiashiria kuwa wapinzani wetu waliweka dawa kwenye vyumba vyetu “- alidai kiongozi huyo wa Polisi Tanzania.
“