Klabu ya Polisi Tanzania yenye maskani yake jijini Moshi-Kilimanjaro imeendelea kujiimarisha kupitia dirisha dogo la usajili kwa kumungeza mlinda mlango katika kikosi chao.
Maafande hao wamemsajili mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Simba na Singida Utd Manyika Jnr kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Ligi Kuu nchini Kenya.
Taarifa zinathibitisha Manyika Jnr amejiunga na Polisi Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea katika klabu ya KCB ya nchini Kenya.
Manyika Jnr alietokea Simba B kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa pia amepita katika klabu ya Singida United kabla ya kutimkia Kenya aliposajili misimu miwili iliyopita akiwa na Jamal Mwambeleko!