Sambaza....

Kikosi cha Polisi Tanzania kimeanza Kambi ya siku 10 katika shule ya maafisa wa Polisi Dar es Salaam Kurasini (DPA) kujiwinda na michezo miwili iliyo mbele ya ligii kuu ya NBC dhidi ya Namungo na Yanga.

Baada ya kumalizika kwa michezo miwili ya Ligi kuu ya NBC ya nyumbani dhidi ya Mtibwa na Biashara wachezaji walipewa mapumziko ya siku 7 ambayo yamemalizika hapo jana na leo wachezaji wa kikosi hicho wameanza mazoezi katika uwanja wa shule ya maafisa wa Polisi chini ya kocha Mkuu Malale Hamsini.

Kutokana na umuhimu wa michezo hii miwili katika kusaka alama tatu, uongozi umeona ni vyema kuweka kambi eneo ambalo hali ya hewa yake haitofautiani na Lindi na timu itapata utumivu wa kutosha kabla ya kwenda Lindi kuwakabili Namungo mchezo utakaochezwa Juni 16 uwanja wa Ilulu saa 10 alasiri.

Polisi Tanzania inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu ya NBC ikiwa imejikusanyia alama 33 baada ya kucheza michezo 26 ikiwa imesaliwa na michezo 4 dhidi ya Namungo, Yanga, Geita na Kagera. Michezo mitatu ikiwa ni ya ugenini na wa Geita ukiwa wa nyumbani utakaochezwa katika uwanja wa Ushirika.

Sambaza....