Sambaza....

Kocha wa timu ya Machester City Pep Guardiola amesema mafanikio ya Ligi ya Mabingwa ya Manchester City “uliandikwa mbinguni” baada ya timu yake kufanikiwa kuifunga Inter Milan na kutwaa mataji matatu mjini Istanbul.

City iliifunga Inter Milan 1-0 na kushinda taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa katika historia yao, na kuongezea  zaidi ya taji la Ligi Kuu na Kombe la FA ambayo tayari walikuwa wametwaa msimu huu.

“Nimechoka, nimetulia na nimeridhika. Ni vigumu sana kushinda, Iliandikwa kwenye nyota. Ni yetu,” alisema Guardiola, ambaye pia alishinda alishinda mataji matatu akiwa na Barcelona.

Bao la kiungo Rodri dakika ya 68 – bao lake la pili katika Ligi ya Mabingwa katika mechi 48 – lilitosha kuwafunga Inter Milan kwenye Uwanja wa Ataturk Olympic, Istanbul Uturuki.

“Inaleta hisia . Ndoto imetimia. Vijana hawa wote hapa walisubiri sijui ni miaka mingapi,
Wanastahili, tunastahili. Miaka iliyopita tulikuwa karibu sana. Nataka tu kumshukuru kila mtu. Haikuwa rahisi. Ni timu gani tuliyokutana nayo, jinsi wanavyolinda na kushambulia,” Rodri aliiambia BT Sport

“Tulifanya kila tunachoweza. Fainali ni kama hii. Huwezi kutarajia kucheza vizuri sana kama kawaida. Hisia ziko. Tumeshindana kama wanyama. Ni ndoto. Wakati huu hautatokea tena.”

Manchester City walikuwa wakishiriki fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa ndani ya misimu mitatu, baada ya kushindwa na Chelsea mwaka 2021.

Sambaza....