Sambaza....

Kwanza tunaanza kumtazama Pep Guardiola namna alivyokijenga kikosi cha Manchester city aina ya uchezaji kwenye kikosi chake.

Pep ni moja kati ya walimu wajanja sana, ukiangalia kikosi cha Manchester city namna kinavyocheza licha ya kumsukuma mpinzani kurudi kwenye eneo lake, lakini pia imekuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kwenye eneo la 14 la kiwanja hapa unaweza kuwaona watu kama Rahim Sterling, Kelvin De Bruyne na Reloy Sane wamekua wakipiga pasi nyingi kuelekea kwenye eneo hili.

Ni aina ya uchezaji ambao umempa mafanikio makubwa sana Pep tangu akiwa na kikosi cha Barcelona, na mara nyingi huitaji wachezaji wenye kasi, wanyumbulifu na uwezo mkubwa wa kupiga pasi

Baada ya kuangalia hayo ebu turudi kwenye mada yangu ya msingi. KWA NINI PEP ANAMUHITAJI ALEXIS SANCHEZ?

Kiufundi Manchester city hutumia sana mfumo wa 4-3-3 huku kwenye flame yake ya juu uwepo watu kama Leroy Sane, Rahim Sterling hawa mara nyingi hucheza kama washambuliaji wanaotokea pembeni na hili ndilo eneo ambalo Pep anahitaji kumuongeza Sanchez

Akiamini ataongeza wigo mpana kwenye eneo la ushambuliaji ukizingatia Gabriel Jesus ni injury prone na Sergio Alguero bado hajarudi kwenye ubora wake tangu apate ajali, lakini pia uzoefu wa Sanchez utaongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji hasa pale atakapohitaji kuipeleka timu kwenye wide formation huyu ni mtu sahihi anayeweza kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha

Rotation kwenye kikosi

Hapa Pep anamuhitaji Sanchez kumrahisishia kwenye hili bila kuathili uchezaji wa timu, ni mchezaji anayeingia kwenye maeneo mengi katika safu ya ushambuliaji

Pep ni mwalimu anayependa kushinda mataji mengi kila msimu hivyo kwa kulitazama hilo anahitaji upana wa kikosi chake

Sambaza....