Simba inaondoka leo hii kuelekea Lubumbashi nchini Congo ƙkwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya TP Mazembe.
Kwa mujibu wa Meneja wa timu hiyo Patrick Lweyumamu amedai kuwa msafara wa Simba utaondoka na ndege maalumu ya kukodi.
Amedai kuwa Simba itaondoka na jumla ya msafara wa watu 30 ambapo wachezaji watakuwa kumi na nane tu na viongozi nane pamoja na benchi la ufundi.
Meneja huyo alikuwa anazungumza na mtandao huu wa Kandanda.Co.Tz baada ya kumaliza mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mechi ya marudiano.
Pia Meneja huyo ametoa taarifa ya Pascal Wawa kukosekana katika mchezo huo wa marudiano baada ya kuumia katika mchezo wa awali uliomalizika kwa suluhu hapa nchini.