Aliyekua kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Pape Osmane Sakho ametoa ya moyoni baada ya kuachana na klabu yake hiyo na kutimkia nchini Ufaransa.
Pape Sakho amejiunga na klabu ya Youville Metropole inayoshirikia League II nchini Ufaransa akiuzwa na Simba kwa dau la zaidi ya biliono mbili.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Pape Sakho amewaaga Simba akiandika “Ni vigumu sana kusema kwaheri. Ulikuwa uamuzi mgumu kufanya, lakini soka ndivyo hivyo. Jambo muhimu zaidi kwangu ni kwamba sisi tayari ni familia, na mmeniunga mkono kila wakati,” alisema na kuongeza.
“Sina hata maneno ya kuelezea jinsi nilivyo na huzuni. Nadhani katika soka ni kujaribu kupanda viwango, lakini fahamu kuwa Simba Sc bado ni familia yangu. Wanasimba, ninawaona kila mahali, na ninataka kusema asante kwa upendo wenu. Naipenda Simba, na itakuwa hivi daima.”
“Ipo siku nitawaeleza wanangu maana ya Simba. Asante sana, na ninatamani timu ishinde kila kitu. Shukrani kwa wachezaji wote, viongozi wa Simba, kocha na wafanyakazi wote. Vikombe vyote, InshaAllah. Shukrani kwa klabu yangu mpya Queville Routine Metropole kwa kunipa nafasi ya kwenda kiwango cha juu zaidi. Kwaheri, familia,” alimalizia Sakho
Pape Sakho atakumbukwa na mashabiki wa Simba pamoja na Watanzania kwa ujumla baada ya kuandika historia kwa Simba na Tanzania baada ya kuchaguliwa kwa bao lake na kuwa bao bora la Afrika msimu wa 2021-2022.
Mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Senegal alifunga bao hilo katika mchezo wa hatua ya makundi kati ya Simba na Asec Mimosa katika Dimba la Benjamin Mkapa.