Sambaza....

Naaaam soka hushangaza, soka huduwaza mashabiki hususani matokeo yake. Katika soka kuna ukatili ndani yake, ufundi, juhudi nidhamu na maandalizi. Kama ijulikanavyo soka huwa na matokeo yake ( kushinda, sare, na kupoteza).

Tangu msimu huu umeanza YANGA katika (NBC PREMIER LEAGUE 2024/25) umekuwa mzuri katika michezo yao nane ya mwanzo kwa kushinda mechi hizo zote bila kuruhusu bao. Ili onekana kama msimu ulio bora zaidi kuwa wamejizatiti kushinda na bila kuruhusu bao kiasi cha kuwafanya waimbwe katika kila kona ya mitaa. Baada ya hapo wakapoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Azam Fc pale Chamazi Complex na dhidi ya Wafuga nyuki wa Tabora (Tabora United) hapo hapo Chamazi Complex.

Kupoteza michezo miwili mfululizo kumezua gumzo, maswali yaliyokosa majibu kwa mashabiki na wafuasi wa Yanga. Lakini ni furaha isiyo na kifani kwa mahasimu/wapinzani wao katika ligi. Kupoteza huku mara mbili mfululizo kumeibua mijadala mingi kiasi cha Yanga kubadili uwanja na kuhamia KMC complex wakibadili upepo pengine matokeo yanaweza kuwa mazuri kwa mechi zijazo.


Mtandao wa Kandanda.co.tz umekuandalia majibu/ sababu za kiufundi na zisizo za kiufundi zilizonyuma ya kipigo mfululizo kwa Yanga na pengine zinaweza kuendelea kuwatafuna YANGA na kuwasababishia vipigo vingine vingi huko mbeleni.

> Lazima tukubali kuwa timu nyingi Tanzania (NBC premier league) ziko na nidhamu ya mchezo hususani wanapocheza na Yanga. Unapocheza na Yanga ni lazima ujiandae, ni kama fainali. Juhudi, kujitoa na motisha (POSHO) lazima iwe kubwa ili kuweza kukabiliana na yanga barabara. Kwamfano mchezo dhidi ya Tabora ambao Yanga walipoteza kwa magoli matatu kwa moja, mkuu wa mkoa wa Tabora aliahidi millioni 30 kama motisha endapo watamfunga yanga, na baada ya mchezo alipandisha bonasi mpaka millioni 100 kama zawadi ya ushindi. Lakini pia wadau wa soka Dar es salaam wametoa karibia millioni 60. Hii inaonyesha ni kwa namna gan ahadi, na motisha zilikuwa kubwa kiasi cha kuwafanya Tabora wapambane sana, lakini walijiandaa vizuri na walichangamka na kushinda mechi.

> Ugumu wa ratiba – Ratiba ya mechi za ligi imekuwa ngumu sana kwa Yanga. Wakiwa na wastani wa kucheza mechi kila baada ya siku mbili. Ugumu ratiba ndio unapelekea mabadiliko makubwa ya kikosi( ROTATION KUBWA). Ugumu wa ratiba unapelekea wachezaji kupata fatiki (kuchoka kupita kiasi) na kusababisha udumavu wa viwango kitu ambacho kimechagiza yanga kupoteza michezo miwili mfululizo.

Kocha mpya wa Yanga Miguel Gamondi akiwa mazoezini na wachezaji wake

> Majeraha na kadi – Yanga inakumbwa na rundo la wachezaji wa kikosi cha kwanza wenye majeraha pamoja na kadi. Hivyo walilazimika kuwachezesha wachezaji wasio katika kikosi cha kwanza na katika nafasi sahihi. Kwamfano mechi dhidi ya Tabora united ambapo walipoteza kwa mabao matatu kwa moja safu ya ulinzi ya Yanga ilionekana kuwa na mianya sana na hii imetokana na kuwakosa wachezaji wake vinara. Kutokuwepo kwa wachezaji wake muhimu katika safu ya ulinzi kama vile kouasi Attoula, shedrack boka(majeraha) na kukosekana kwa Dickson job na Ibrahim Bacca (kadi) na nafasi zao kuchukuliwa na Denis Nkane, Aziz Andambwile (ambaye pia aliumia na kutolewa) kiasili wachezaji hawa sio mabeki na sio wachezaji wa kikosi cha kwanza lakini walilazimika kucheza na kupelekea kupoteza. Mchezo dhidi ya Azam kadi nyekundu ya Ibrahim Bacca kipindi cha kwanza cha mchezo ilipelekea yanga kucheza pungufu kwa dakika nyingi na kupoteza kwa kufungwa goli moja kwa bila.

Msimamo wa Ligi kwa Timu Tano

PosTimuPWDLGDPts
1Azam FC1510321533
2Simba SC1210112131
3Yanga SC1210021330
4Singida BS149321130
5Tabora Utd FC15744025

> Mahusiano mabovu kati ya benchi la ufundi na baadhi ya wachezaji – wapo baadhi ya wachezaji hawana mahusiano mazuri na kocha suala ambalo limekuwa likitoa ufinyu wa kikosi mfano mahusiano mabovu kati ya Kibwana shomari na benchi la ufundi. Kibwana alikuwa mchezaji muhimu na wakutegemewa ambaye angeisaidia timu katika kipindi hiki lakini sababu ya mahusiano mabovu na kocha amejikuta akisugua benchi. Suala hili linaigawa timu kwani sio kila mchezaji atakaa upande wa kocha, wengine wataona ni uonevu hivyo watakosa ile morali ya kumpambania kocha na timu kwa ujumla.

> Yanga wanatabirika kirahisi – Hivi karibuni Yanga wamezoeleka kutumia mipira mirefu ambapo mpira ukitoka kwa kipa (Diara) hupelekwa ma mabeki wa kati (Job/Bacca/Mwamnyeto) hupigwa pembeni kulia au kushoto mwa uwanja, mabeki wa pembeni hushambulia kwa kupiga krosi na washambuliaji kufunga. Kila mechi wamekuwa wakitumia mbinu hii hivyo wapinzani hujipanga vyema kwani ni mbinu ambayo huitumia mara zote. Na hata wakitawala mchezo kwa kumiliki mpira kwa kupiga pasi fupi fupi kunawapa nafasi na muda wapinzani kujipanga vizuri kuzuia.

Na hili limeonekana katika mechi dhidi ya Azam na ile ya Tabora united ambazo zote alipoteza. Ile yanga iliyozoleka ya kukaba kwa nguvu na kufanya mashambulizi ya kushitukiza haipo tena kwani hawajaionesha hadi sasa hivi. Kwani kuna baadhi ya misingi msimu uliopita ilikuwa inawapa matokeo mazuri na kuwafanya kuwa hatari kwa kila mchezo msimu huu haipo.

Ni lazima tukubali kuwa kama MIGUEL GAMONDI atasalia kuwa kocha wa Yanga ni lazima apambane vya kutosha kuhakikisha misingi kadhaa inarudi na makali ya yanga yanarudi.
UKIONA VYA ELEA UJUE VIMEUNDWA na kandanda.co.tz imeundwa ili kuhakikisha unapata majibu ya maswali yako, usisite kututembelea www.kandanda.co.tz.

Sambaza....