Sambaza....

Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC imefikia raundi ya tano kwa timu zote katika makundi yote kushuka dimbani mara tano huku stori kubwa ikiwa ni mshambuliaji wa Yanga Kenedy Musonda.

Baada ya kuiongoza Yanga kuvuka hatua ya makundi na kwenda robo fainali kwa kufunga bao moja na kutengeneza goli la pili la Mayele na kupelekea Yanga kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya US Monastir sasa Kenedy Musonda ndio mchezaji aliehusika kwenye mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo.

 

Kenedy Musonda sasa amehusika katika mabao matano ambapo amefunga mabao mawili na kutoa pasi tatu za mabao katika michezo mitano ya Yanga kwenye kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika orodha hiyo Musonda anafwatiwa na Abdala El Said wa Pyramids mwenye goli moja na pasi tatu za mabao hivyo kuhusika katika mabao manne sawa na A. Kramo wa Asec Memosa mwenye mabao manne. 

Katika orodha hiyo tatu bora ya wachezaji waliohusika katika mabao mengi inafungwa tena na mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele mwenye mabao matatu na pasi moja ya bao na hivyo nayeye anahusika katika mabao manne.

Kenedy Musonda akimuacha mlinzi wa Real Bamako

Kufanya vyema kwa nyota hao wa Yanga kunawafanya  Wananchi kushika nafasi ya tatu katika timu zenye mabao mengi katika michuano hiyo.

Yanga wana mabao nane yakufunga mpaka sasa wakiwa sawa na Pyramids ya Misri wakizidiwa na Malumo Gallants na Rivers United wenye mabao tisa huku vinara wakiwa ni FAR Rabat wenye mabao kumi.

 

Sambaza....