- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Kiungo wa klabu ya Simba Haruna Niyonzima amedai kuwa kwa sasa amerudi kwenye kiwango chake cha awali, akizungumza na mtandao huu amedai kuwa mazoezi yamemrudisha kwenye ubora wake.
“Nilikuwa nje kutokana na kuumwa. Lakini nilifanya mazoezi baada ya hapo. Na hizi mechi ambazo nimezipata zimenisaidia kurudi kwenye kiwango changu”
Alipoulizwa anakizungumziaje kiwango chake katika michezo ambayo amecheza kanda ya Ziwa , Haruna Niyonzima amedai kuwa angalau kwa sasa anajiona yeye.
“Mazoezi na hizi mechi ambazo nimezipata hivi karibuni ndizo zimenifanya nifanye vizuri katika michezo ambayo nimecheza katika kanda ya Ziwa”.
Alipoulizwa kama ratiba ya Simba itakuwa kikwazo kwenye mbio za ubingwa kiungo huyo amedai kuwa watalambana kuhakikisha wanatetea ubingwa.
“Ratiba ni ngumu sana lakini tumejiandaa kutetea ubingwa huu na kuhakikisha kuwa na msimu huu tutakuwa mabingwa wa Tanzania bara”. Alidai kiungo huyo kutoka katika ardhi ya Paul Kagame, nchini Rwanda.