Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa leo tarehe 15 November. Klabu ya Simba imepokea majina ya wachezaji watano kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Assumes ambao wanatakiwa kupelekwa kwa mkopo katika timu mbalimbali.
Moja ya majina ambayo yapo kwenye orodha hiyo ni jina la kiungo wa klabu hiyo Haruna Niyonzima. Ambaye alisajiliwa kutoka kwa mahasimu wao Yanga.
Inasemekana kuwa kiungo huyo raia wa Rwanda ameomba kama anatakiwa kupelekwa kwa mkopo basi apelekwe katika klabu yake ya zamani Yanga.