- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
–Makala hii iliwekwa katika tovuti hii tarehe 29/09/2013. Imewekwa tena leo wakati tovuti ikisheherekea miaka 8. Iliandikwa na Oscar Oscar Jr-
Hivi karibuni ilipigwa PWANI DERBY pale mabatini stadium JKT RUVU VS RUVU SHOOTING hatukusikia malalamiko ya uwanja, Prison vs Mtibwa imepigwa siku si nyingi Sokoine stadium, sikusikia malalamiko ya uwanja.
Anyway, ukiondoa shamba la bibi, uwanja wa Taifa na ccm-Kirumba, viwanja vyote vilivyobaki haviko kwenye hali nzuri. Kila timu inayotoka Dar siku hizi wasipopata point 3 tu mikoani, lawama zote ni kwenye ubovu wa viwanja!!
Tuache uwongo! Mchezaji wa kitanzania anauwezo wakucheza hata juu ya mti mradi tu magoli yawepo. Huko Dar kwenyewe hamna kiwanja, mnatumia cha Taifa na “Nipige tafu” toka Azam Complex.
Nina wasiwasi siku SIMBA VS YANGA wakijenga viwanja vyao, wanaweza kuomba TFF ili mechi zao zote za nyumbani na ugenini zichezwe kwenye viwanja vyao maana vya mikoani vibovu.
Timu yetu ya Taifa mechi zote tangu kupatikana kwa hilo GODORO STADIUM, zinapigwa hapo na vitasa tunakula hapo hapo!!
I’m sorry namsubiri Kim Poulsen nae siku moja aseme kama tatizo ni uwanja ili tujenge mwingine!