Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga ambaye alisajiliwa msimu huu na kutemwa msimu Juma Balinya amedai kuwa wakati yuko Yanga kulikuwa na michezo ya kishirikina aliyofanyiwa na wachezaji wenzake.
Mchezaji huyo ambaye alikuja Yanga akiwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda , amedai kuwa kuna baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wanafanya michezo hiyo ili yeye asifanikiwe.
Akizungumza na mwandishi wetu nchini Kenya ambako jana alifanikiwa kuingia mkataba mpya na GorMahia ya Kenya , mkataba wa mwaka mmoja alidai kuwa moja ya sababu iliyofanya asifanye vizuri ni michezo hiyo.
“Kuna michezo michafu ambayo ilikuwa inafanyika na Mimi nilikuwa mhanga wa hilo ila kwa sasa nataka kuangalia mbele kwa ajili ya kuitumikia GorMahia” amedai mchezaji huyo