Kocha mkuu wa Tanzania, Mnigeria, Emmanuel Amunike amekiri kuwa Tanzania haijaifikia Nigeria licha ya kufuzu kwenda AFCON mwaka huu. Amunike ameyasema haya wakati akihojiwa moja kwa moja na kituo cha SuperSport 9 katika kipindi cha Naija Made.
Amunike aliulizwa anamaoni gani kwa uwezekano wa Tanzania kupangwa na timu yake ya taifa ya Nigeria. Ndipo alipojaribu kuelezea kuwa, kitu muhimu ni Tanzania kufuzu haya mashindano lakini akakiri kuwa Nigeria ni wazoefu zaidi yetu ‘..Nigeria has more expirience than Tanzania…’, sehemu ya nukuu ya maneno yake.
Amunike aliwashangaza na kuwachekesha waendesha kipindi baada ya kusema ‘Tumefuzu…’ na Watangazaji wakacheka na kumjibu kuwa sisi ni Wanigeria sio Watanzania.
Hakika inaweza kuwa ni mchezo mzuri na wa kuvutia kama Tanzania itakutana na Nigeria, lakini tutegemee nini?. Hata kama Nigeria wanauzoefu mkubwa AFCON tutakutana na timu zenye uzoefu huo huo, hatuna budi kupambana.