Sambaza....

Klabu ya soka Yanga leo imeingia na makubaliano na benki ya CRDB kudhamini wiki ya Wananchi ambayo kilele chake kitakua ni July 22 mwaka huu.

Katika hafla ya kutia saini iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa benki ya CRDB ilihudhuriwa na Mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga Andrew Ntine, mkuu wa kitengo cha kadi benki ya CRDB Farid Seif na kaimu mkurugenzi wa wateja binafsi Stephane Adil.

Kwenye hafla hiyo adhimu kabisa mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga alisema “Hili ni tukio maalum la kusaini mkataba na benki ya CRDB kuelekea katika wiki ya Wananchi,” alisema na kuongeza.

Viongozi wa Yanga na CRDB Benki wakitia saini mkataba wa ushirikiano wa Wiki ya Wananchi.

“Itakua wiki maalum kwasababu itajumuisha viti vingi maalumu na vizuri, Ally Kamwe atawaelezea. Kila kitu ni maalumu katika wiki hii ya Mwananchi lakini zaidi natangaza siku maalum zaidi ambayo ni siku ya kuhitimisha ambayo tutacheza na Kaizer Chiefs. Ni klabu kubwa yenye historia kubwa kama Yanga. Itakua ni mchezo mzuri kwa timu zote mbili lakini pia kwa mashabiki.

Nae kaimu mkurugenzi wa wateja binafsi CRDB Stephane Adil alisema “Tulikua tunatafuta jinsi ya kuwafikia wateja wetu na tukaona ushirikiano na Yanga ndio sahihi kwetu ili kiwafikia Wananchi. Yanga imekidhi vigezo kitaifa na kimataifa na ndio maana tunashirikiana nao.”

“Sisi CRDB pia tupo Congo DR na Burundi hivyo hapa Wakimataifa tumekutana na tunaamini huu ushirikiano utakwenda vizuri. Kwa udhamini huu tunajua tunawapunguzia gharama maana kuendesha hizi timu zinahitaji pesa nyingi.”

Sambaza....