Sambaza....

Wananchi Young Africans, kwa mara ya kwanza imeanzisha enzi mpya kwa kusaini mchezaji kutoka Afrika Kusini na kuwa wakwanza kufanya hivyo katika nchi hiyo za Afrika Mashariki baada ya kukamilisha usajili wa Mahlatsi Makudubela kutoka Marumo Gallants.

Usajili wa nyota huyo wa PSL ni wakati muhimu kwa soka la Tanzania na ishara ya kukua kwa soka la Tanzania barani humo. Rais wa Yanga, Hersi Ally Said amewahi kusema wanamtolea macho mwanasoka kutoka Afrika Kusini. “Lengo kuu ni sehemu ya mpira wa miguu. Tunahitaji mchezaji ambaye anaweza kutupa matokeo uwanjani,” Said aliiambia FARPPost walipokua wakifanya mahojiano.

Mahlatsi Makudubela Skudu katikati ya walinzi wa Orlando Pirates.

“Pili, pia ni ushirikiano wa mashabiki kuunda mahusiano mazuri ya klabu nje ya nchi. Tutakuwa na idadi ya mashabiki kutoka Afrika Kusini ambao watashawishika kumsapoti mchezaji wao.”

“Kwa hivyo, ndio, sababu za kwanza ni za mpira wa miguu na nambari ya pili ni ushiriki wa mashabiki na kuunda uhusiano kati ya klabu na wafuasi nje ya nchi.”

Hata hivyo imefahamika Yanga walimkosa mchezaji wake chaguo la kwanza Ranga Chivaviro, ambaye Kaizer Chiefs ilimnyakua.

Sambaza....