Kandanda Chat inakuletea maoni tofauti kutoka kwa wasomaji wetu, dokezo hili likiandikwa na Raymond Mlowe (Shabiki wa Azam FC na Arsenal FC).
Gadiel Michael ni Mchezaji wa daraja la juu na amecheza mechi Karibu zote za Timu ya Taifa na yupo kwenye umri sahihi. Ni kweli anawekwa Bench na Mohamed Hussein (ambaye naye ni bora) .Hakuna dhambi kuwachukua wote wawili hata kama wanatoka timu moja. Kujaribu left back mpya kwenye mashindano ni jambo la kustaajabisha kidogo. Na si lazima tulazimishe Kibabage acheze ili Jadida wamwamini. His time will come.
Soma pia:
Nani chaguo sahihi kiufundi: Tshabalala/ Gadiel?. Sehemu ya 1.
Nani chaguo sahihi kiufundi: Tshabalala/Gadiel? Sehemu ya Pili
Eliuter Mpepo: Sijui jicho la Kocha liliona nini kule Kampala. Lakini binafsi niliona alifanya kazi kubwa kiasi cha kujikatia tiketi ya Kuitwa kikosini. Lakini kumuacha yeye na kujaribu mshambuliaji mpya (Reliant Lusajo) ni kamari nyingine.
Frank Raymond Domayo “Chumvi” . Dah! Mwalimu eeh! Kama umemuacha Mudathiri basi punguza gambling na mjumuishe huyu mwamba. A complete box to box midfielder. Au ndo kusema Himid, Bryson na Sure boy wanatosha;wasijesema kiungo cha Azam tupu?
Kwani lazima Mchezaji wa Polisi awepo? Mlianza kutalii na Majogoro. Nchimbi kahamia Yanga. Leo mmekuja na Sabilo. Kweli Stars ya wote Ila siyo muda wote.
Makipa wanne?? Anywayz Najua mtapunguza kwenye final submission.
Kila lakheri Taifa Stars.