Sambaza....

Mrisho Khalfan Ngassa jina ambalo liliandikwa katika mioyo ya mashabiki wa Yanga, ni ngumu kulifuta katika mioyo yao kwa sababu mhuri wa moto ulitumika kuweka chapa ya jina la Mrisho Ngassa kwao.

Chapa ambayo ilitokana na kiwango cha wakati huo cha Mrisho Khalfan Ngassa, kiwango ambacho ƙkilimpa heshima ambayo ilimfanya awe kipenzi cha wanaYanga wengi.

Uwezo wake wa kukimbia na mpira ilikuwa burudani iliyotengeneza tabasamu zito kwenye nyuso za mashabiki wa Yanga, chenga zake za maudhi zilitengeneza kelele za kumsifu Ngassa na magoli yake yalitengeneza shangwe za kushangilia kwa nguvu.

Hapo ndipo ulikuwa mwanzo wa yeye kuwa kipenzi cha wanaYanga. Hapana shaka alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuchezea mpira kwa sababu ya sanaa kubwa ya mpira aliyokuwa nayo pamoja na uwezo wa kufunga magoli.

Alifanikiwa kushindana na washambuliaji halisi wa kati katika ufungaji wa magoli, kwa kifupi Mrisho Khalfan Ngassa kilikuwa kipaji kilichokamilika.

Kipaji ambacho kiliweka ufalme wake kipindi kile kina nguvu kubwa ya kukimbia kwa kasi na kufunga magoli.

Kila kitu kwenye maisha ni msimu, msimu wa Mrisho Khalfan Ngassa kucheza katika kiwango cha juu tayari umeshapita.

Tangu arejee kutoka Afrika Kusini na kujiunga Mbeya City baadaye Ndanda FC hajaonesha kiwango kikubwa kama alichokuwa nacho awali kwa sababu kasi yake imepungua kwa kiasi kikubwa kama kipindi kile.

Anakuja Yanga, kutakuwa na faida kwa Yanga? Hapana shaka Yanga watanufaika naye kutokana na malengo yao ambayo yaliwafanya wamchukue.

Wamemchukua kama nani ?, kama mchezaji wa ambaye anategemewa kuleta mabadiliko ndani ya uwanja kwa kufunga magoli kama awali? hapana shaka hii ni ngumu kwa Yanga kunufaika katika mlango huu kwa sababu hata takwimu za Mrisho Ngasaa msimu huu hazimbebi kufanya kitu kama hiki.

Hivo Yanga walitakiwa kuangalia namna bora ambayo ingewafanya wanufaike na Mrisho Khalfan Ngassa.

Mrisho Khalfan Ngassa ni mchezaji mzoefu aliyewahi kucheza katika kiwango cha ushindani ƙkwenye mechi za kitaifa na kimataifa na anaijua vizuri Yanga kwa sababu aliitumikia kwa muda mrefu.

Hii ilitosha kwa Yanga kumtengeza Mrisho ƘKhalfan Ngassa ƙkuwa kocha wa baadaye kwa Yanga kwa kuanza kumpa nafasi kama kocha mchezaji wa Yanga.

Uzoefu wake, mafanikio yake aliyoyapata kwenye mpira , mafanikio ambayo yamempa heshima kubwa , heshima ambayo ingetumika vizuri sana kuwaonesha wachezaji wa kikosi cha Yanga umuhimu wa kuipigania timu kwa ajili ya manufaa yao binafsi na manufaa ya timu husika.

Sambaza....