Siku ya jana nilizama kwa mawazo ya maswali ambayo majibu yake hadi muda huu sijayapata, anaandika Matukuta JR, shabiki wa Yanga kutoka Mbeya, endeleakusoma hapa.
Kocha Mwinyi Zahera ameendelea kuwa mkweli juu ya wachezaji wake na uongozi wa timu yetu ya Yanga.
Kile alichokisema jana kwa uchungu kocha Zahera ndio maisha halisi ya Yanga kwa sasa, tumekuwa na uongozi wa kisanii ambao unatupa faraja kwenye paji la uso huku ndani ya mioyo yao wanalia.
Kwanini nimewataja wakina Msumi na Kaisi? Hawa wameenda kwenye vyombo vingi vya habari wakipinga mchakato wa uchaguzi hasa kwa nafasi ya Mwenyekiti wakisema Manji bado ni Mwenyekiti wa Yanga.
Swali la kujiuliza Manji ni mwenyekiti kivuli au jina la Manji linatumika hili baadhi ya watu wanufaike kwa faida yao binafsi au linatumika kukwamisha baadhi ya watu wanaohitaji kuifadhili au kuiongoza Yanga?
Kocha Zahera anakwambia hayupo Yanga kwa ajili ya fedha ila kwa ajili ya mashabiki wa Yanga ambao ni kipenzi chao.
Sasa tujiulize amedanganywa Zahera au mashabiki na wanachama wa Yanga?
Kocha ametoa mapendekezo kwa viongozi wahusika(lawama zote kwa Nyika) hadi siku 1 kabla ya dirisha kufungwa unamwamvia kocha mambo yote sawa bt siku ya mwisho unamwambia mambo yameshindika.
Nani asiyejua Yanga tunahali ngumu ya kiuchumi?
Kama suala lilikuwa ni pesa hawa wakina Lukumay na Nyika walimwambia nani?
Je walishirikisha wanachama kama ambavyo tulichangia bukubuku za awali?
Anyway sasa turudi kwenye hili la Manji(alituzoesha jeuri ya fedha) je alishirikishwa juu ya mapendekezo ya kocha juu ya usajili.
Na yeye kama Mwenyekiti alitoa maoni au ushauri gani?
Hapa ndio tunapokubaliana na wengi ambao tunataka Yanga ifanye uchaguzi wa kuziba nafasi zote kuanzi Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wote.
Hii hali imekuwa na usanii tuna kikosi kidogo sana na hata performance yetu iko chini kiasi tunapata matokeo kwa shida sana(morali ya wachezaji imetusaidia) chini ya umakini wa kocha Zahera.
Sasa kwa nini hatutaki kufanyia kazi ushauri wake?
Yanga hii imesajili hadi golikipa ambaye hakuwa kwenye mipango ya kocha tena inasemekana ni golikipa HURU aliyedaka kwenye Beach Soccer ya Timu ya Taifa Zanzibar.
Hitimisho:
Kwasasa Yanga inahitaji uchaguzi kuliko Manji kama Mwenyekiti Kivuli.
Na kama kocha Zahera ataondoka basi waliomfukuza ni kina Hussein Nyika kutofuata ushauri wa mapendekezo yake juu ya usajili.