Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Ihefu na Simba utakaopigwa kesho jioni nahodha wa Simba Mohamed Hussein ametamba kuendeleza ushindi mbele ya Ihefu “Mbogo Maji”

Mlinzi huyo wa kushoto wa Simba amesema anajua Ihefu wataingia uwanjani wakitaka kulipiza kisasi baada ya kuwafunga mabao matano katika robo fainali ya FA.

 

Mohamed Hussein ” Haitakua rahisi sana Ihefu ni timu nzuri na jambo lingine litakalofanya mchezo kuwa mgumu ni kutokana tumwafunga juzi kwahiyo na wao watataka kulipa kisasi,” alisema na kuongeza

“Kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuja kutupa sapoti, sisi wachezaji tupo kamili kuhakikisha alama tatu zinapatikana,” alimalizia.

Nae kocha wa Simba Robertinho Oliveira amesema walipata ushindi juzi lakini huu ni mchezo mwingine wa Ligi ambao wanahitaji kuwa bora.

 

“Ni kweli tumewafunga juzi lakini hii mechi ni nyingine, kuna dakika tisini mpya  za kuthibitisha ubora uwanjani,” alisema  Robertinho Oliveira

Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na alama zao 57 katika msimamo wakati Ihefu wao wanashika nafasi ya 6 na alama zao 33 katika msimamo wao wa Ligi Kuu ya NBC.

Sambaza....