Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amebakisha mwaka mmoja pekee katika mkataba wake na Yanga huku ofa kibao zikimiminika Jangwani lakini kocha wake Nasraddine Nabi amesema atakapokwenda.
Koch Nabi, ametaja ofa kadhaa kutoka Afrika Kusini, Mashariki ya Kati na Ulaya ambao wapo katika harakati za kuhitaji huduma yake. “Nimefurahishwa sana na kiwango ambacho Fiston amekuwa nacho katika klabu kwa sababu nilikuwa sehemu ya kusajiliwa kwake kutoka AS Vita,” Nabi alisema na kuongeza “Tumemwona akiendelea na kiwango kizuri, lakini kwa bahati mbaya kuna ushindani mkubwa. Anatafutwa kila mahali Afrika Kusini, Saudi Arabia, Ufaransa, na labda hata Ubelgiji.
Nabi amesema Mayele amekua lulu na ili kumpata inahitajika klabu yenye misuli yakifedha kuendana na dau lakumpata kutokana na vilabu vingi kumuhita.
“Ni mchezaji mzuri na ili kumfikisha hapa Afrika Kusini, labda, utalazimika kulipa pesa nyingi sana – anahitajika mno,” alisema Nabi aliyeipeleka Yanga fainali ya Kombe la Shirikisho.
Kufuatia kufanya kwake vyema katika michezo ya Kombe la Shirikisho Mayele amekua akihitajika kila kona na kwa Afrika Kusini Kazier Chiefs wameonekana kumuhitaji nyota huyo kutoka Congo DR.