Mzamiru Yassin fundi wa mpira asiyepewa ‘thamani’ stahiki na mashabiki.
Usipo kuwa na jicho la kiufundi huwezi kuona mchango wake wa moja kwa moja kwa kuwa play style yake haina ‘mbwembwe’ hajui na hajajaliwa nakshi nakshi nyingine.
Mara nyingi viungo wasio na ‘udambwidambwi’ kama ndugu yangu hapa huwa hawajikusanyii mashabiki kama wale wachezea mpira kama ilivyokuwa Mpwa wangu @shakhanrashid na wengineo wengi.
Lakini kuna kazi ya kifundi ambayo Mwamba huyu huwa anakifanya ambaye siyo rahisi sana kuona kwa jicho lisilo la kiufundi.
Mwamba anaiendesha timu ana toa kile viungo wengi mafundi hawana uwezo wa kufanya hasa kwenye kukaba na kupora mipira kwa wapinzani na kuirejesha kwenye timu yake
Wale wachezeshaji wanaosifika ndani ya timu pale mpira unapokuwa wao shughuli unapokuwa kwa wapinzani lakini Mwanaume huyu ni Mwamba haswa
Binafsi akiwa kwenye timu yangu pettern ya uchezaji ingeanzia kwakwe na timu ingekuwa bomba sana.
OK any way kwenye Koti la Babu sijakuacha mikono mitupu (swipe kushoto) uchungulie kuna nimekuwekea za leo na kesho kama huna kifua basi chukua za leo tu hapo