Mshambuliaji wa kimataifa wa Sierra Leone, Musa Noah Kamara maarufu kama ‘Musa Tombo’ aliyezaliwa August 06, 2000 maeneo ya Tombo nchini Sierra Leone, alikimbizwa hospitalini baada ya kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu tumboni.
Musa Tombo amekuwa akitoa kauli za kutishia kujiua hasa baada ya kusitisha mkataba wake na klabu ya Al-Ittihad ya Libya na kusimamishwa na chama cha cha Soka nchini Sierra Leone kutokana na matukio yake ya utovu wa nidhamu.
Baadhi ya matukio ya Mussa Tombo
-Musa mwenye umri wa miaka 22 ameshidwa kabsa kucheza soka nje ya Sierra Leone sio kwa sababu ya kipaji ni kwa sababu zake mwenyewe mara ya kwanza alipelekwa Sweden kwenye klabu ya Trelleborgs FF baada ya kusajiliwa akakataa kwa kusema kuna baridi na kuanza kulia siku nzima siku ya pili wakala wake akamua kumrudisha nyumbani kwao Sierra Leone.
-Kuna wakala mmoja alijitokeza na kumpeleka nchini Norway kwenye timu ya ligi kuu alisajiliwa bila hata kufanyiwa majaribio Musa baada ya kushinda siku moja akaanza kulia na kulalamika akitaka arudishwe kwao wakala akadai wamuache tu atazoea, Musa akaendelea kulia na akatishia kujinyonga iwapo hawatamrudisha kwao wakala huyo akamurudisha haraka kwao Sierra Leone.
-Kijana huyu wakasema labda ameshindwa kucheza soka nje ya Afrika, Mwezi wa nane (August) alisajiliwa na klabu ya Al Ittihad Tripoli ya Libya akaenda kujiunga na klabu ya hiyo baada ya siku 6 tu akaomba kurejeshwa nyumbani kwao Sierra Leone kwa madai ya kuwa anasikia milio ya bastola usiku nchini Libya hivyo haoni usalama wa kutosha.
-Musa Noah Kamara Tombo akavujisha video fupi akiwa ameshika panga akiwa anasema endapo atauliwa (atakufa) akiwa nchini Libya basi wakala wake Roland Ekokobe na mke wake (Hawa) wanastahili kushitakiwa na kubeba lawama zote kwani alikuwa amekata tiketi ya kurejea nyumbani kwao Sierra Leone wao waka i-cancel tiketi yake.
-Baada ya Mikasa ya kutaka kujiua Mussa alivunja mkataba wake na klabu ya Al Ittihad Tripoli ya Libya akarejea zake nyumbani.